Fahamu kuwa si kwa sababu unataka kusoma nje ya nchi basi kila nchi ni salama kwako, hapana baadhi si salama kwako na baadhi ni salama kwako kutokana na vigezo na mazingira mbali mbali.
Kwa mtu ambaye una ndoto za kutafuta elimu nje ya nchi ya Tanzania, una kila sababu ya kusoma makala hii.Kadhalika mtu ambaye una shauku la mwanao au jamaa yako asome nje ya nchi taarifa hizi zawezakuwa za muhimu sana kwako.Chanzo cha makala hii ni gazeti la Mtanzania.
KILA mtu anatamani kusoma nje ya
nchi hususan Ulaya ambako baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kuwa kusoma au
kupata ujuzi kwenye vyuo hivyo vya ng’ambo kutawawezesha kupata fursa
zaidi za ajira ikilinganishwa na kusoma kwenye vyuo vya ndani.
Kumekuwapo baadhi ya changamoto
ambazo zimekuwa zikiwapata wanafunzi wa kigeni pindi wanapokuwa ng’ambo.
Hii inatokana kwamba nchi nyingi
zimekuwa haziweki mazingira mazuri kwa wanafunzi wa kigeni, hata inapotokea
wamekumbwa na misukosuko serikali za nchi hiyo zimekuwa zikichelewa kuchukua
uamuzi au kuwatetea wanafunzi hao.
Hali hiyo imekuwa ikichangia baadhi
ya wanafunzi na wazazi kuwa na hofu ya kwenda kusoma nje ya nchi zao.
Matukio kadhaa yasiyo ya kufurahisha
yamewakumba wanafunzi wa kigeni, hali hiyo imekuwa ikitafasriwa kama ni kawaida
kwa mataifa yaliyo na vyuo bora nje ya nchi jambo ambalo si kweli.
Kama ndoto zako au hata za mtoto
wako ni kusoma na kupata ujuzi nje ya nchi kwenye vyuo vilivyoendelea na
kujenga wasifu wake vizuri utakaomsaidia kupata kazi kirahisi ndani na nje ya
nchi na bado hujajua ni nchi gani ambayo mwanao atasoma akiwa salama na
kukarimiwa vizuri, makala hii itakupa mwanga.
Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Ulaya
EU miezi michache iliyopita, imeorodhesha nchi nane zinazoongoza kwenye
kuwakarimu wanafunzi wa kigeni.
Uingereza
Nchi hii imepata asilimia 0.7 ya
kukarimu wageni huku ikinyakua asilimia 0.5 ya wanafunzi wanaohitimu kwenye
vyuo vyake.
Licha ya kwamba nchi hii iliibuka
kinara kwa kuwa na wanafunzi wengi wa kigeni kati ya nchi 35 za bara hilo
lakini ilikuwa na asilimia 40 ya wanafunzi wake ambao walihitimu nje ya vyuo
vya nchi hiyo kwa mwaka 2012-2013 jambo ambalo lilifanya ipunguziwe alama
kwenye ripoti hiyo.
Mbali na ‘doa’ hilo, ni wazi kuwa
Uingereza imekuwa ikisifika kwa kuwa na mazingira mazuri kwa wanafunzi wa
kigeni ikiwamo kuwapa msaada wa karibu na kuwashirikisha kwenye fursa
mbalimbali za kiuchumi.
Ubiligiji
Ina asilimia 2.4 ya ukarimu kwa
wanafunzi huku kiwango cha wanafunzi wanaohitimu masomo yao nchini humo kikiwa
ni asilimia 3.3 ambapo pia imekuwa ikisifika kwa kuwahamasisha wananchi wake
juu ya watoto wao kujifunza lugha za kigeni walau 15 kwa mwaka.
Nchi hii haijapishana na Uingereza
katika kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi sanjari na kuwawezesha kiuchumi
ambapo katika kulitekeleza hilo imekuwa na mikakati mbalimbali ukiwamo ule wa
‘Flemish community’ wenye lengo la kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020
inakuwa na asilimia 33 ya wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali wanaokwenda
kusoma nchini humo.
Kwasasa asilimia 48 ya wanafunzi wa
kigeni wanaosoma nchini humo ni kutoka Ufaransa.
Denmark
Hii ina asilimia 1.3 ya ukarimu kwa
wanafunzi huku ikiwa na asilimia 1.7 ya wanafunzi wa kigeni wanaohitimu kwenye
vyuo mbalimbali nchini humo.
Denmark ni miongoni mwa nchi chache
za Ulaya zinazotoa msaada mkubwa zaidi kwa wanafunzi wa kigeni karibu wote
wanaofika kuchukua masomo yao nchini humo, pia inatoa ushirikiano zikiwamo
taarifa mbalimbali kwa wanafunzi.
Pamoja na mambo mengine imeweka
mkazo wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anajifunza lugha mbili kwa wakati
mmoja kwa kipindi cha walau miaka mitano huku akipata mkopo na msaada mkubwa
kutoka serikalini.
Nchi nyingine ambazo zimekuwa na
alama za juu zaidi ni pamoja na Ujerumani ambayo ina asilimia 3.9 ya kukarimu
wanafunzi wa kigeni huku ikiwa na asilimia 54.1 ya wanafunzi wa kigeni
wanaohitimu masomo yao nchini humo.
Lakini pia imekuwa ikitoa misaada ya
hali na mali kwa wanafunzi wote wa kigeni wanaofika nchini humo. Nyingine ni
Bulgaria yenye ukarimu wa asilimia 7.8 kwa wanafunzi wa kigeni na asilimi 6.6
ya wanaohitimu. Asilimi 52 ya wanafunzi wake wanatoka nchini Uturuki.
Nyingine ni Uholanzi, Luxembourg na
Slovakiam. Chaguo ni lako mwanafunzi na mazazi kumpeleka mwanao nje au la kwani
nchi hizo zote zina mazingira rafiki ya taaluma na hali ya juu
MRMWALIMU.BLOGSPOT.COM#ELIMU KWANZA
0 Comment to "NCHI NANE KINARA WA KUWAKARIMU WANAFUNZI WA KIGENI"
Post a Comment
Post a Comment
1410