Kumekuwa na matukio mengi ya vitendo vya ushirikiana ambavyo huwalenga walimu.Baadhi ya maeneo walimu wakipangiwa hawakai kwa sababu ya vitendo vya kishirikina. Ni jambo la kusikitisha sana maana linaathiri sana walimu na elimu kwa ujumla maana ni wanafunzi ndiyo wanakosa elimu.Hatuwezi sema serikali ipambane na vitendo hivi bali tunasema jamii ibadilike.Chanzo cha habari hii ni gazeti la Mwananchi.
Ukerewe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Frank
Bahati amesema wafanyakazi 46 wa wamewasilisha maombi ya kuhamishwa kwa kuhofia
ushirikina.
Bahati amesema
kuwa maombi hayo yamewasilishwa kwa miezi kumi tangu mwaka huu uanze.
“Tunaendelea na
uchunguzi kuhusu sababu za maombi haya, hatua za kisheria zitachukuliwa iwapo
itabainika kuwa watumishi hawa wanatumia madai ya vitendo vya ushirikina kwa
ajili ya kupata uhamisho nje ya wilaya,” ameonya Bahati.
Amefafanua kuwa
katika uchunguzi wa awali imebainika kuwapo kwa baadhi ya wazazi wilayani humo
kutumia vitisho vya ushirikina dhidi ya watumishi wanaowabana kwa makosa
mbalimbali ikiwamo utoro.
Hivi karibuni
Shule ya Msingi Uhuru ilifungwa baada ya walimu kuacha kuingia darasani
wakishinikiza kuhamishwa kutokana na hofu ya ushirikina.
Walimu hao walidai
mwalimu mwenzao, Obadia Bwatwa alianguka ghafla na kufa wakati akirejea
nyumbani kutoka shuleni.
Tangu kifo hicho
kitokee Oktoba 23, mwaka huu, walimu hawajaingia darasani kufundisha baada ya
kuingiwa hofu wakiamini kifo cha mwenzao kilitokana na ushirikina.
Hata hivyo,
Mkurugenzi huyo amekanusha kifo hicho kutokana na ushirikina akisema uchunguzi
wa kitabibu umebaini kuwa mwalimu Bwatwa alikuwa na ugonjwa wa moyo.
0 Comment to "Ushirikina kikwazo kingine cha maendeleo ya elimu yetu"
Post a Comment
Post a Comment
1410