Mwalimu ni mzizi
wa elimu. Uboreshaji wa elimu unapaswa uaanzie kwenye mizizi ya elimu ambao ni
walimu. Kinyume na hapo tutafanya mengi lakini elimu itazidi kushuka.
Mr.Mwalimu Blog tunaamini ni wakati wa kila mwenye mawazo ya kuboresha elimu
ayaseme ili tuwe na mjadala wakitaifa kuhusu uboreshaji wa elimu.
Ndugu Benedecta
Mrema ,afisa habari na utetezi wa Hakielimu ni miongoni mwawanaharakati
wazuri wa suala la kuboresha elimu. Ni mtu anayejua anachokisemaa, anakisema
kwa kujiaamini akiambatanisha namifano halisia mingi ya kitafiti na kihistoria.
Ameandika makala haya katika gazeti la mwananchi, kwa kuwa ana hoja nzito zenye
mwelekeo wa kuboresha elimu mimi naibandika hapa makala hii hapa Mr.Mwalimu Blog
Mwaka 1966,
Mwalimu Julius Nyerere alisema, nanukuu.
“Wale wenye wajibu
wa kufanya kazi na vijana wa umri mdogo wana nguvu kubwa zisizozidiwa na nguvu
za yeyote yule kwa kutilia maanani hali ya baadaye ya jamii yetu. Nguvu hizi
zipo katika makundi mawili, wazazi na walimu.”
Ukisoma hotuba
zake nyingi, zimezungumzia kwa kina masuala ya elimu kama mkombozi. Mwalimu
alieleza wazi kuwa, lengo la kwanza la elimu ni kumkomboa mtu binafsi na taifa
kutoka kwenye kutegemea mataifa yaliyoendelea kiuchumi na kiutamaduni.
Aidha, elimu
inapaswa kumjengea mhitimu maarifa, stadi na uwezo wa kukabiliana na changamoto
za maisha halisi anayoishi.
Katika kufanikisha
lengo hili la elimu, mwalimu alitaja katika nukuu hapo juu kuwa kuna makundi
mawili ambayo yana nguvu kubwa ya kuwafanya wanafunzi kufikia malengo ya kuwapo
shuleni. Makundi haya ni wazazi na walimu.
Tafiti nyingi
zilizofanyika katika kubaini sababu za kushuka kwa ubora wa elimu zimekuwa
zikijikita katika kuangalia masuala kama miundombinu isiyofaa ya kufundishia na
kujifunzia. Ni tafiti chache zilizolenga kuangalia ubora wa walimu na mazingira
yanayomzunguka.
Pia, tafiti hizo
zinaonyesha wazi kuwa watoto wetu hawajifunzi licha ya kuwa wanakwenda shuleni.
Kwa mfano, siyo jambo la kushanganza kuona watoto wakimaliza darasa la saba
bila kujua kusoma na kuandika.
Jitihada
zilizofanyika kujaribu kuinua kiwango cha ubora wa elimu haziwezi kupuuzwa hata
kidogo. Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya jitihada kubwa kuinua
kiwango cha ubora wa elimu yetu, lakini bado hatujaweza kupata matokeo
yanayotakiwa kama ambavyo wadau wengi walitarajia.
Lazima tukubali
kutafuta mzizi halisi wa tatizo la kushuka kwa elimu yetu. Pengine tatizo
linafahamika lakini nia ya kushughulikia tatizo siyo makini.
Kimsingi,
tumechelewa kushugulikia kiini cha tatizo kiasi kwamba Tanzania ya viwanda na
ya uchumi wa kati tunayoitaka kufikia mwaka 2025, inaweza kuishia midomoni kama
hatutaamua kuchukua hatua mapema.
Wadau wengi wa
elimu wameshasema kuwa kuwathamini walimu ni moja ya hatua ya kurejesha ari ya
ufundishaji kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, yaani enzi za Mwalimu Nyerere.
Kuanzia ngazi ya
taifa mpaka familia, walimu hawaonekani tena kama watu muhimu; wanachukuliwa
kama watu maskini waliokosa cha kufanya na ndiyo maana wapo huko.
Mwalimu mmoja
aliwahi kusema: “Kuna wakati wanafunzi wananiuliza, “Mwalimu, una akili, lakini
sasa kwa nini uliamua kuwa mwalimu?” Maswali ya aina hii yanakera. Ina maana
wanaamini mwalimu ni mtu aliyefeli, asiye na akili.
‘’Ninapowaambia,
nilipenda tu kuwa mwalimu”, wananiambia huoni kwamba unachelewa katika maisha?
Haya ndiyo maisha tunayoishi katika shule hii.’’
Ni dhahiri kuwa
huu ndiyo mzizi wa tatizo la kushuka kwa ubora elimu yetu. Miundombinu ni
muhimu katika kujifunza na kufundisha, lakini pasipo walimu bora wenye moyo na
hamasa ya kufundisha kamwe hatutofikia elimu bora tunayoitaka.
Utafiti uliofanywa
na shirika la HakiElimu mwaka 2011 usemao: Je? Walimu wana sifa za ualimu na
hamasa ya kufundisha?, pamoja na mambo mengine ulibianisha kuwa mwalimu kuwa na
sifa nzuri za kitaaluma pekee bila kuwa na hamasa na moyo wa kujitolea
hakusababishi kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi kitaaluma kuimarika’
Benedicta Mrema ni
ofisa programu Idara ya Habari na Utetezi, HakiElimu media@hakielimu.or
0 Comment to "UCHAMBUZI: Mwalimu akithaminiwa elimu yetu itapanda chati"
Post a Comment
Post a Comment
1410