Matokeo ya utafiti yaliotangazwa na taasisi ya Twaweza yanahitaji utafiti zaidi ili kuthibitisha.Kwa macho ya kawaida haionyeshi kuwa ubora wa elimu umeongezeka bali idadi ya wanafunzi imeongezeka. Tumeongeza idadi ya wanaohudhuria shule lakini hatujaongeza ubora. Habari hii imeandikwa na gazeti la Mwanachi.
By Raymond Kaminyoge, Mwananchi
Dar es Salaam. Taasisi ya Twaweza imefanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 50 ya wananchi waliohojiwa wanasema ubora wa elimu umeongezeka tangu mfumo wa elimu bila ada ulipoanzishwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza,Aidan Eyakuze amesema idadi hiyo ya wananchi ni kati ya 1806 waliohojiwa Tanzania Bara.
Amesema asimilia 35 wamesema ubora umebaki palepale na wengine asilimia 15 wamesema ubora umeshuka.
Utafiti huo umefanyika kati ya Agosti 7 na 14 mwaka huu.
Hata hivyo baadhi ya wasomi wamesema kiwango cha elimu hakiwezi kuboreshwa katika kipindi kisichofikia mwaka mmoja.
0 Comment to "Utafiti: Elimu bure imeongeza ubora wa elimu"
Post a Comment
Post a Comment
1410