Mwalimu una nafasi ya kuzuia matukio
ya aina hii yasiendelee. Ni kweli kuwa kuna wakati wanafunzi wanaudhi
kupindukia lakini imetupasa kujizuia hasira zinapokuwa juu dhidi ya wanafunzi.
Matukio ya namna hii yakiendelea taswira ya taaluma ya ualimu itachafuka na
kuonekana kama genge la watesaji wa wanafunzi.Chanzo cha habari hii ni gazeti la Mtanzania.
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari
Ridhwaa Seminary iliyopo wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Yusuph Kivugo,
amemshambulia mwanafunzi wake, Mbaraka Mwalimu, kwa kumpiga ngumi usoni na
kumsababishia maumivu makali.
Mwanafunzi huyo anayesoma kidato cha
nne katika shule hiyo iliyopo Kinondoni Mkwajuni, alikutwa na mkasa huo Novemba
3, mwaka huu wakati akijiandaa na mtihani wa Historia.
Kwa mujibu wa ratiba ya mitihani ya
taifa ya kidato cha nne inayoendelea nchini, mtihani huo ulikuwa unafanyika
mchana, lakini hata hivyo hakufanya kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.
“Tulikuwa msikitini na wenzangu
tunasoma, ilikuwa ni saa mbili asubuhi kabla ya mtihani wa Historia kuanza,
mwalimu alikuja akauliza kwanini tunapiga kelele na kuanza kutupiga.
“Upande wa pili kulikuwa na
wanafunzi wa pre-form one ndio waliokuwa wakipiga kelele, nilishangaa kamkunja
mwenzangu anaitwa Mohamed akawa anampiga mangumi, mimi nilijua labda kuna kosa
amefanya.
“Katika kujitetea akina Mudy
walikimbia, mara akaja kwangu akanishika akaanza kunishambulia, amenipiga ngumi
nyingi za usoni, kwenye taya na nyingine jichoni kiasi kwamba sikuweza kufanya
mtihani kwani jicho lilivimba sana,” alisema.
Mwalimu wa nidhamu shuleni hapo,
Omary Ikome, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema jukumu lake ni kusimamia
nidhamu kwa wanafunzi na kwamba suala hilo lipo juu ya uwezo wake.
“Nilimkuta Mbaraka analia na jicho
la kushoto limevimba, nilimuuliza akasema amepigwa na mkuu. Mimi nasimamia
nidhamu kwa wanafunzi, lakini kwa kuwa kitendo hiki kimefanywa na bosi wangu,
siwezi kuzungumzia zaidi kwani lipo juu ya uwezo wangu,” alisema.
Mwalimu mkuu huyo alipoulizwa kiini
cha tatizo, hakuweza kutoa ushirikiano na kumfukuza mwandishi ofisini kwake.
0 Comment to "Mwalimu Mkuu ampiga mwanafunzi ngumi za uso."
Post a Comment
Post a Comment
1410