Iko fursa adhimu sana ya kujiendeleza kielimu kwa wafanya
kazi, wafanyabiashara, wakulima, wazee na vijana, wanawake na hata wanaume
ambayo haijafahamika kwa watu wengi. Watu wa chache waliyobaini fursa hii ya
kujiendeleza kitaaluma wameitumia, wanaitumia na watataiendelea kuitumia kadiri
ya hali, uwezo na mahitaji yao. Mr. Mwalimu Blog
inakufafanulia
Na kwa ukweli halisia
watu waliyoitumia fursa hii ndoto zao kimaisha zimetimia, maisha yao kikazi, kibiashara
na kiuchumi hayajabaki vilevile, wamekuwa watu wengine, elimu imebadilisha
maisha yao hata wamekuwa watu wenye thamani kubwa na manufaa ya mapana na ya
kina kwa jamii hata nchi.
Kwa kuwa fursa hii ni ya thamani, ina nguvu ya kubadilisha
maisha ya watu wengi kwa wakati mmoja lakini haifahamiki kwa wengi, nimeona
niandike ufahamu wangu mdogo juu ya fursa hii ambayo imekuwa kama ardhi yenye
dhahabu ambayo iko katika makazi ya watu ambao hawatambui kama udongo wanao
ukanyaga una utajiri mkubwa!
Huenda kupitia andiko
hili watu mbalimbali wataamsha shauku ya kujiendeleza kielimu, watarejesha
matumaini ya kujiendeleza baada ya kukata tamaa kutokana na vikwazo mbali mbali
vya kimazingira, kikazi, au kiuchumi hatimaye nchi ikanufaika kupitia
kujiendeleza kwao.Mr. Mwalimu Blog inakufafanulia
Nchi hii ingali ina uhaba mkubwa wa wasomi, ndiyo maana watu
wenye kujiendeleza kielimu wana nafasi nzuri ya kuwa viongozi katika mazingira
yao ya kazi, katika jamii na hata katika nchi. Elimu bado ni ufunguo wa
mafanikio wenye thamani kubwa katika ulimwengu na katika nchi ya Tanzania. Kwa
mantiki hiyo, elimu inaongeza thamani ya mtu hivyo kila mtanzania anapaswa
kufikiri namna atakavyojiendeleza kielimu.
Elimu haina mwisho, kuridhika na kiwango fulani cha elimu,
ni kasumba mbaya inayodumaza mafanikio ya wengi pia inadumaza ustawi wa Taifa.
Watanzania ni miongoni mwa watu wenye kasumba ya kutojishughulisha sana
kujiendeleza kielimu hasa baada ya kupata kazi inayokidhi mahitaji yao.
Tuna watu wengi wenye uwezo wa kujiendeleza kielimu
hawafanyi kwa sababu ya kuridhika kupindukia, kwa sababu ya kutokufahamu
umuhimu wa kujiendeleza au kwa sababu ya kukatishwa tamaa na mazingira na
taratibu za kazi wanazofanya.Mr. Mwalimu Blog inakufafanulia
Matokeo ya hali hii ni kwamba kuna baadhi ya watumishi wa
serikali wakiwemo walimu, wahudumu wa afya, maskari, maafisa maendeleo n.k
ambao wana zaidi ya miaka kumi wakiwa na kiwango kile kile cha elimu ambacho
walianza nacho kazi miaka mingi iliyopita.
Kwa kweli kuna watumishi ambao wanaanza kazi mpaka
wanastaafu bila kijiendeleza kielimu, hivyo kuna watu wanafanya kazi miaka
thelathini na kustaafu akiwa na kiwango kile kile cha elimu alichoanza nacho,
yaani kama alianza kazi miaka ya sabini akiwa na stashahada anastaafu leo akiwa
na stashahada ile ile!
Wakati watumishi wengi wakisita kujiendeleza kielimu kwa
sababu mbalimbali ambazo kwao ni za msingi, watumishi wengine wa serikali na wa
umma wanajiendeleza kitaaluma kila mchwao. Mathalani wako watumishi
walioajiriwa wakiwa na elimu ya kidato cha nne, leo wana astashahada, stashahada,
shahada na hata baadhi wana shahada za uzamili! Hivyo hata hawako tena katika
nafasi za kazi walizoanza nazo, wala hawako katika madaraja ya mishahara
waliyoanza nayo. Wako katika nafasi za juu kiutendaji, wapo katika madaraja ya
juu ya malipo na maisha hayako vile vile.Mr. Mwalimu Blog inakufafanulia zaidi;
Kama wewe ni mtumishi wa umma au sekta binafsi, ambaye
umejiandaa kustaafu ukiwa na kiwango hicho hicho cha elimu ulichonacho leo,
kama wewe ni mtu mwenye kiwango fulani cha elimu na haujafikiria kukiongeza kwa
sababu mbalimbali za kulaumu watu, wazingira au kujitetea, naomba nikuombe
ubadilishe mtizamo wako, nakuanzia sasa ufikirie kujiendeleza kwa sababu ipo
nafasi ya kujiendeleza. Chemchemi hiyo ya kuichotea elimu itayotoa maji ya
kumwagilia ndoto zako, ziote,zistawi na hata zizae matunda ni Chuo kikuu Huria
cha Tanzania.
Katika mazingira ya sasa licha ya kwamba mwamko wa elimu si
mkubwa lakini watu wachache wanaopenda
kujiendeleza kielimu wanakutana na vikwazo vingi sana katika kutimiza ndoto
zao. Moja ya kikwazo ni sheria na taratibu za utumishi wa umma ambazo zinataka
mtu kuomba kwenda masomoni baada ya kutimiza miaka mitatu ya utumishi.
Ugumu zaidi unakuja kwa sababu hata baada ya kutimiza miaka
mitatu, mazingira ya kupata ruhusa kwenda masomoni yanabaki kuwa magumu. Kwa
nini? Kwa sababu wanaoomba kwenda kusoma katika baadhi ya taasisi na idara ni
wengi hivyo ruhusa utolewa kadiri ya uwezo na uhitaji wa taasisi. Na wakati
mwingine mazingira ya rushwa na upendeleo huusika pia ili kupata ruhusa hizo
kutoka kwa watendaji wao wakuu.
Watu wenye kupenda kujiendeleza kitaaluma lakini kazi
wanazofanya zinawabana, wana nafasi ya
kujiendeleza kupitia elimu ya masafa, wale wenye kuweza kupata muda saa za
jioni wanaweza kutumia muda huo kujiendeleza kupitia mfumo wa madarasa ya jioni
kila siku katika Chuo kikuu Huria.Mr. Mwalimu Blog inakufafanulia kwa kina.
Mfumo mwingine wa utoaji wa elimu katika chuo kikuu Huria ni
mfumo maalumu(Exacutive) ambapo wanafunzi wa taaluma fulani ukusanyika mkuo fulani
kwa kipindi cha siku kadhaa wakifundishwa na wahadhiri makini wa chuo kikuu
Huria na kisha hurejea makwao. Ukifahamu jinsi Chuo hiki kinavyotoa elimu bora
kwa bei nafuu na kwa njia au mazingira rahisi basi hauna sababu ya kukaa na
kiwango kile kile cha elimu miaka nenda rudi.
Chuo kikuu Huria cha Tanzania ni miongoni mwa vyuo bora nchini
ambacho hivi sasa kinatumiwa na watu mpaka nje ya nchi ikiwemo nchi za Zambia
Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi, Misri n.k kinatoa nafasi ya kujiendeleza kwa
bei nafuu kadiri ya muda wako. Ni chuo ambacho kila mtu anaweza kukitumia
kujiendeleza kwa kuwa kinatoa elimu ya taaluma mbali mbali kuanzia ngazi za
astashahada,stashahada, shahada, shahada za uzamili na hata za uzamivu.
Ikiwa fursa hii
inawanufaisha mpaka watu wan je ya nchi, vipi wazawa tunaoizunguka chemchemi ya
elimu tusijinufaishe nayo. Tuseme ni kweli ,kwamba, penye miti hapana wajenzi
na upele umuota asiye na kucha?
Katika wakati huu ambao serikali ni kama imebana zaidi mazingira
ya watumishi wake kupata fursa ya kujiendeleza, kutokana na kuweka masharti
magumu kwa watu wanaotaka kwenda kusoma, kama vile, watumishi watakaokwenda
kusoma wawe wametimiza miaka mitatu ya utumishi, watumishi watakao enda
masomoni kutokupandishwa madaraja, katika mazingira mengi watumishi watakaoenda
kusoma watalazimika kusitishiwa asilimia kumi ya mishahara yao au kusitishiwa
mshahara.Mr. Mwalimu Blog inakufafanulia uelewe.
Chuo kikuu Huria cha
Tanzania ni fursa pekee ya kufanya usome huke ukiendelea na kazi hivyo kulinda
maslahi yako kama mfanyakazi, ni fursa ya kujiendeleza hata kwa watumishi ambao
hawajatimiza miaka mitatu kazini. Hakuna sheria inayombana mtumishi
kujiendeleza kielimu kupitia chuo kikuu cha Tanzania.
Tunao viongozi na watu wa kawaida walioitumia fursa ya chuo
kikuu Huria, kujiendeleza mfano mzuri ni Waziri wa Tamisemi wa sasa George
Simbachawene, kwa kweli ni mtu mtu anayestahili kupongezwa sana kwa bidii yake
ya kujiendeleza kielimu kutoka ngazi ya chini kielimu hata akahitimu shahada ya
sheria katika chuo kikuu Huria. Job Ndugai, spika wa Bunge la jamuhuri la
Muungano, makamu wa Rais wa sasa Samia Suluhu Hassani na wanasiasa na viongozi
wengine wengi ni miongoni mwa walioiona fursa ya chuo hiki na kuitumia kwa
manufaa.
Jambo moja linalonivutia sana waziri mkuu wa sasa, Mh.
Kassim Majaliwa, ni historia yake kielimu, ameanzia ngazi ya cheti
(astashahada), akajiendeleza huku akifanya kazi mpaka kufikia kuhitimu shahada
ya uzamili, na hivyo pia tunao walimu wa UPE waliofanya mafunza ya elimu kwa
muda mfupi ili kuondoa changamoto ya uhaba wa elimu wakiwa ni wahitimu wa
darasa la saba tu lakini leo hii ni wahitimu wa astashahada,stashahada, shahada
na hata shahada za uzamili na uzamivu.
Watumishi wa umma, watumishi wa sekta binafsi na watu wote
tuhamasike kujiendeleza kielimu. Ulimwengu huu ni ulimwengu wa elimu fikiria na
amua kujiendeleza, weka kando visingizio sehemu ya kujiendeleza kwa gharama
nafuu, kwa mazingira rahisi na ukapata elimu bora ipo.Mr. Mwalimu Blog inakufafanulia tena
Kama viongozi wetu wa ngazi mbalimbali wanaweza kujiendeleza
kielimu licha ya majukumu mengi waliyonayo, wewe unakosaje hamasa na nafasi ya
kujiendeleza. Zinduka, acha visingizio, tumia fursa chuo hiki kujiendeleza.
Wakati huu, mtu anayefanya kazi miaka kumi bila kwenda kujiendeleza kielimu
kiasi akastaafu akiwa na elimu ile ile aliyoanza nayo ni uzembe wa kutumia
fursa.
Mr.Mwalimu.Blogspot.com.
mrmwalimu@yahoo.com,
0746492600
0 Comment to "CHEMCHEMI YA KUJICHOTEA MAFANIKIO KWA WATUMISHI NA WATU WOTE"
Post a Comment
Post a Comment
1410