Monday, October 31, 2016

UVUJAJI WA MITIHANI TENA?

Kama kuna mfupa ambao Baraza la mtihani chini wizara ya elimu imeushindwa kuutafuna kwa miongo kadhaa sasa basi ni uvujaji wa mitihani ya kitaifa. Mitihani ya kitaifa kuanzia darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, cha nne hivyo mpaka cha sita haikosi dalili za kuvuja kila inapofanyika.

Bado      wizara ya elimu haijafanikiwa kudhibiti kasumba hii mbaya na yenye athari nyingi mbaya kwenye elimu. Kadiri siku zinavyozidi kwenda inataka kuonekana kama ni jambo la kawaida kuvujisha mitihani.

Kwa kweli uvujaji wa mitihani unaelekea kuwa sehemu ya utamaduni wa taifa letu. Kila mwaka matokeo yanapotangazwa au mitihani inapofanyika lazima visa vya wizi wa mitihani visikike.Yaani kuvuja kwa mitihani kungekuwa kigezo cha kumuondoa waziri wa elimu au katibu wa baraza la mitihani basi hakuna ambaye angedumu kwenye hizo nafasi kwa zaidi ya mwaka mmoja. Ingekuwa kila mitihani wa kitaifa unaenda na waziri na katibu wake wa baraza la mitihani.

Kwa kiasi kikubwa wahusika wa kuu wa kuvujisha mitihani ni wasimamizi wa mitihani. Visa vingi vya uvujaji mitihani vinavyoripotiwa vinaonyesha wazi wasimamizi wa mitihani kuhusika. Kwa kweli kwa asilimia nyingi mtihani hauwezi kuvuja kama msimamizi hataamua uvuje.

Watawala wa elimu katika wilaya, Walimu wakuu, wamiliki wa shule na wakati mwingine wana bodi ya shule ndiyo wamekuwa wakijihusisha na uvujaji wa mitihani ili kuzipatia shule zao majina. Walimu wakuu wanaojihusisha na vitendo hivi huwahonga wasimamizi wa mitihani kiasi fulani cha fedha ili wakiuke kanuni za usimamizi wa mitihani.

Mathalani kwa mujibu wa baadhi ya walimu waliowahi kuwa wasimamizi katika shule kadhaa, wanasema kuna shule ambazo huandaa kabisa fungu la fedha kwa ajili ya kumpooza msimamizi ili wizi wa mitihani ufanyike.

Kwa hiyo ukosefu wa maadili na uaminifu ni moja ya sababu kubwa sana ya uvujaji wa mitihani, baadhi ya wasimamizi wanageuza kazi ya kusimamia kama sehemu ya kujipatia faida mara mbili, kwa sababu wanalipwa na baraza lakini pia wanalipwa rushwa na wakuu wa shule au wamiliki wa shule.

Uko ujingi hata wa wazazi kuchangisha fedha za kuibia mitihani katika baadhi ya maeneo. Ukweli ni dawa ,tukikaa kimya Taifa litaangamia. Leo hii watoto wanafaulu kwenda kidato cha kwanza huku hawajui hata kusoma na kuandika, unajiuliza mtihani wao walifaulu vipi kama si wizi!

Wasimamizi wa mitihani waliohongwa huwa hufanya ya fuatayo, kwanza hutumia muda mwingi nje ya chumba cha mtihani. Hufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa wanafunnzi kuigiliziana majibu na kupeana majibu.

Wakati mwingine msimamizi wa mitihani wakishahakikishiwa donge nono, hushirikiana na askari wasiowaaminifu kufungua mitihani kabla ya muda, kisha huitafutia majibu na kisha majibu hayo hupewa wanafunzi kabla ya mtihani. Hapa ndiyo kama mlivyosikia hivi karibuni wanafunzi walikutwa wameingia na majibu yaliyoaandikwa kwenye sare zao za shule.

Wapo wasimamizi ambao hutumia mbinu ya kuchukua karatasi ya maswali na kuitoa nje , huko nje walimu wa shule husika hujichimbia kutafuta majibu ya maswali husika, Ambapo majibu hayo hupewa msimamizi awasambazie watoto.

 Kadhalika shule inaweza kuyaweka majibu hayo chooni ili wanafunzi wanaofanya mtihani wakiomba ruhusa kwenda chooni hujue wanarudi na majibu. Wanafunzi wawili watatu wanaweza hata kujifanya wanaharisha, wakaenda chooni mara kwa mara kumbe wanaenda kuchukua majibu. Mr.Mwalimu Blog inashauri upekuzi wakina ufanyike na inapotokea wanafunzi au shule imaiba mtihani kupitia njia hii askari aliyekuwa anasimamia awajibishwe vikali.

Hii inawezekana tu kama askari ambaye anawajibu wakukagua vyoo kabla ya kuanza mtihani, ana wajibu wakumpeleka mwanafunzi chooni na kukikagua choo mara kwa mara atazembea au kama nae atakuwa ametembezewa mlungula.

Uvujishaji wa mitihani ni janga kwa sababu, unaharibu watoto, watoto wanakuwa wazembe kujisomea, wakitegemea mitihani itavuja. Pia inaharibu maadili ya watoto. Fikiri kuhusu mwalimu anaekaa chini na mwanafunzi wakapanga mipango ya kuiba mtihani, akifaulu baada ya myaka akawa mwalimu atakuwa mwalimu wa namna gani.

Janga la wizi wa mitihani linafundisha watoto kutokuwajibika, linafundisha watoto wizi na ndiyo hawa wanakuwa watumishi wa umma alafu haachi kuiba kwa sababu ndiyo njia iliyowatoa.

Mtihani wa kidato cha nne inayoaanza leo, ina nafasi kubwa ya kuibiwa kutokana na hali na mwenendo wa ukali wa serikali ya sasa. Wakuu wengi wa shule za umma wanahofia kupoteza nafasi zao kama watoto watafanya vibaya hivyo baadhi watalinda nafasi zao hata kwa kuiba mtihani. Wakuu wa shule binafsi watafanya ili kulinda soko la shule zao.

Wito wangu kwa serikali , ili kukomesha tabia hii mbaya hatua kali na za wazi zichukuliwe dhidi ya wakuu wa shule, wasimamizi, wazazi, wanafunzi na bodi za shule zitakazojihusisha na wizi wa mtihani. Bado sijasikia hatua kali zinazolenga kukomesha jambo hili kabisa, ni kama serikali inawalea waharibifu wa elimu yetu na taifa letu.

Walimu tulinde maslahi mapana ya nchi, tusiwe wepesi wakununuliwa na vijihela vya mchuzi wakati tunaangamiza taifa, wakati tunajishushia hadhi. Walimu ni chumvi ikiharibika haifai. Watu wa usalama, walinzi na mgambo nao wasimamie kazi hii kwa uaminifu. Niliwahi kupita shule moja siku ya mtihani wa darasa la saba nikakuta mgambo anayelinda usalma wa ufanyaji wa mitihani yuko mtaa wa pili toka shule yake anayosimamia.

Wasimamizi mjitahidi kuvishinda vishawishi. Mathalani kuna mwalimu mmoja alinipa ushuhuda, alienda kusimamia mtihani wa kidato cha nne, baada ya kushawishiwa apokee rushwa ya kuvujisha mtihani na kukataa, alifuatwa na wazee maarufu wa hicho kijii na wazee wabodi kumshawishi ili akubali. Hali ilikuwa ngumu kwake kiasi hata wanafunzi aliokuwa anawasimamia hawakuwa wanamsalimia ni hivyo pia wanakijiji. Hii ni jinsi gani wizi wa mitihani ulivyoota mizizi!

Serikali kwa namna ya pekee ifikiri zaidi namna ya kukomesha jambo hili, na namna moja wapo ni kuboresha maslahi ya walimu na wasimamizi wa mitihani.Yote kwa yote ninachojiuliza ni kwamba je mtihani wakidato cha nne utavuja tena mwka huu? Wakati utatoa jibu. Mr.Mwalimu Blog; Elimu Kwanza.

KILA LA KHERI KIDATO CHA NNE

Sunday, October 30, 2016

Mbunge wa Kibiti awapa morali kidato cha nne

Viongozi lazima kutambua mahitaji ya jamii kwa wakati husika. Mbunge huyu kafanya kitu sahihi kwa wakati sahihi. Wanafunzi zaidi ya mazingira mazuri ya kujifunzia ,wanahitaji ukaribu, wanahitaji kutiwa moyo na kuwaambia tuko pamoja.Hongera Mbunge wa Kibiti.Wabunge wengine waige. Chanzo cha habari hii ni Gazeti la MWANANCHI.

Kibiti. Mbunge wa Kibiti, Ally Seif Ungando ametoa vifaa mbalimbali vya kufanyia mtihani wa kidato cha nne na chakula kwa wanafunzi 800 kutoka shule kumi na moja wanaotarajia kuanza mtihani wa Taifa kesho.
Akizungumza katika utoaji wa vifaa hivyo katika Shule ya Sekondari ya Zimbwini, Ungando amesema lengo la kutoa vitu hivyo ni kuwaondolea wanafunzi usumbufu wa ukosefu wa vifaa hivyo na chakula wakati mitihani yao.
Ungando amesema ametoa vitu hivyo baada ya kubaini kuwepo kwa mapungufu ya vifaa vya kufanyia mtihani kwa baadhi ya wanafunzi na wengine kutokuwa na uhakika wa kupata chakula wakati wa kipindi cha mtihani yao.
"Vifaa hivi vya kufanyia mtihani na chakula hiki, nimevitoa ili kuwaondolea usumbufu wa uhitaji katika kipindi cha mitihani yenu mnayotarajia kuianza Jumanne," amesema.
Mbunge huyo ametoa mchele, maharage, mafuta ya kula, rula, kalamu za wino na mkaa pamoja na nyembe vilivyogharimu zaidi ya shilingi milioni tano.
Shule zilizopokea vifaa hivyo ni Zimbwini, Mchukwi, Mlanzi, Ruaruke, Kikale, Mtanga Delta, Wama, Nyamisati, Mlanzi, Mjawa na Msafiri.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Zimbwini, Harieth Mhadu amesema vifaa hivyo vitaongeza molari zaidi wa wanafunzi hao kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

MWAKA MMOJA: JPM ALIVYOIPANDISHA NA KUISHUSHA ELIMU.

Mwaka mmoja wa utawala wa serikali ya awamu ya tano hauwezi kupita bila kufanyiwa tathimini ya kina jinsi alivyoenenda kadiri ya ahadi alizoahidi, kadiri ya ilani ya chama chake katika uchaguzi na kadiri ya alivyoshughulikia changamoto za wananchi.

Mafanikio na madhaifu ya serikali hii yapimwe kwa kutathimini jinsi ilivyoshughulikia kero sugu za wananchi, jinsi ilivyotekeleza ahadi na ilani yake ya uchaguzi, kadhalika tathimini ijielekeze kwenye ubunifu na utayari wa serikali kushughulikia kero mpya na za dharura.

Tathimini yangu juu ya serikali ya awamu ya tano, itajikita katika kuitazama sekta ya elimu. Sera ya elimu bure ndiyo eneo ambalo jicho langu litajikita zaidi. Sera ambayo imeipaisha sana serikali ya awamu ya tano kiasi hatuwezi kutathimini mafanikio ya awamu ya tano bila kujadili mafanikio ya utekelezaji wa sera ya elimu bure. Utekelezaji wa sera hii kwa vitendo umechangia mafanikio yafuatayo kama Mr.Mwalimu Blog inavyofafanua:

Idadi ya wanafunzi kwa ngazi ya awali, msingi na sekondari imeongezeka kwa kasi. Kwa kweli kama kuna mafanikio ya wazi ambayo serikali ya awamu ya nne imepata basi ni kuongeza idadi ya wanafunzi mashuleni. Watoto waliokosa elimu kwa sababu ya ufukara sasa wana matumaini ya kupata elimu.

Utengenezaji wa madawati umeboresha mazingira ya usomaji. Rais Magufuli amejitahidi sana kushughulikia suala la wanafunzi kukaa chini kutokana na ukosefu wa madawati. Ukosefu wa madawati  umeathiri sana mazingira ya kujifunza na kujifunzia kwa wanafunzi.

Mtoto anayekaa chini wakati anafundishwa na watoto watano waliobanana kwenye dawati moja ambalo hukaliwa na watoto wawili hawezi kuelewa vizuri anachofundishwa.  Awamu ya tano imepigana vita na imeshinda kiasi kikubwa sana vita hii dhidi ya watoto kukua chini. Eneo hili ni eneo ambalo pia serikali inapaswa kupongezwa waziwazi.

Serikali ya awamu ya tano imerejesha uwajibikaji wa watumishi wa umma. Si siri nchi imepita kwenye mpito cha uharibifu wa maadili ya utumishi wa umma na sasa Rais Magufuli na serikali yake wapo kwenye kipindi cha mpito cha kurejesha maadili na uwajibikaji wa watumishi wa umma.

Hili Rais pia kwa kiasi kikubwa amefanikiwa, watumishi wanaheshimu kazi na wanawajibika hivyo walimu kama sehemu ya watumishi wa umma, upepo huu wa matengenezo unawakumba pia. Walimu wengi sasa wanahudhuria katika vituo vyao vya kazi na wanawajibika. Haya ni mafanikio ya kujivunia na kupongezwa ndani ya kipindi hiki cha mwaka mmoja.

Ulipaji wa posho za madaraka kwa wakuu wa shule, walimu wakuu na waratibu wa elimu. Serikali imetekeleza moja ya dai la muda mrefu la walimu kutaka kuwepo na posho ya madaraka. Katika kuanza kutekeleza dai hilo, serikali imeanza kuwalipa wakuu wa shule posho ya madaraka ya shilingi 250000, walimu wakuu shilingi 200000 na waratibu shilingi 250000. Haya ni mafanikio yanayoweza kuchagiza kiwango cha elimu. Ni mafanikio kwa sababu wakuu hawa watajituma zaidi na watawawajibisha zaidi walio chini yao.

Kama wasemavyo waswahili penye mafanikio hapakosi changamoto, jitihada zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa ili kuboresha elimu hazijafanikiwa kwa kwa asilimia mia. Hizo Mr.Mwalimu Blog, tunaziita changamoto kwa sababu zinaweza kutatuliwa, si mambo yaliyoshindikana kabisa bali ni mambo tu yanayohitaji dhamira ya kweli katika kuyashughulikia:

Changamoto kuu katika kipindi cha mwaka mmoja cha awamu ya tano ni uhaba wa walimu. Uhaba wa elimu ni miongoni mwa sababu kubwa sana inayodhoofisha elimu yetu. Mathalani katika shule ambayo nafundisha, shule imeanza mwaka 2013 hivyo mwaka huu inatoa wanafunzi wa kwanza wa kidato cha nne lakini Tangu imeanzishwa haijawahi kuwa na mwalimu wa somo la Fizikia!

 Katika miaka minne ya kuwepo kwake imekuwa na walimu wa Baiologia na Kemia kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu pekee. Kutoajiri walimu. Licha ya changamoto walizo kabiliana nazo, kitendo cha serikali ya tano kutoaajiri mwaka 2016 kimeathiri sana elimu. Uhaba wa walimu uliopo ungepungua kama serikali ingeajiri walimu mapema  mara tu baada ya kuhitimu vyuo badala ya kuwaacha waranderande mtaani.

Sera ya elimu bure imetengeneza hali ya kubweteka kwa wazazi, baada ya kutangazwa elimu bure wazazi wengi sasa wanafikiri kila kitu kitafanywa na serikali. Wazazi wengi wasio na uelewa wamejitoa kwenye nafasi zao za kuwawezesha vijana wao, kuwahamasisha kusoma, jukumu hilo wamewaachia walimu. Hivyo elimu ni bure lakini watu hawana msisimko wa kusoma na kusomesha. Ni kama sera hii ya elimu bure imewafanya baadhi ya wazazi kuwa kupe.

Sera ya elimu bure imeathiri utoaji wa elimu, ubora wa elimu na uendeshaji wa shule hivyo kuathiri ubora wa elimu. Kila mwezi Serikali inatoa kiasi fulani cha fedha kufidia ada ambayo ilikuwa inatozwa kwa wanafunzi. Uendeshaji wa shule ambao ulikuwa ukitegemea sana michango ya wanafunzi, sasa unategemea ruzuku na fidia ya ada. Kwa kiasi kikubwa elimu bure imenufaisha wazazi au walezi lakini imeathiri uendeshaji washule na ubora wa elimu.

Kupitia michango ya wanafunzi, shule ambazo hazina walimu wa baadhi ya masomo hususani yale ya Sayansi ambayo yana uhaba mkubwa, shule ilitumia fedha ya taaluma iliyokuwa ikichangwa na wanafunzi kuajiri walimu wa muda. Hivyo pia shule nyingi za msing  zilitumia walimu wengi wa kibarua cha muda kufundisha madarasa ya juu na hata darasa la awali. Shule ziliweza kufanya mitihani yenye ubora kwa kuwa fedha zilikuwepo.

Kwa sababu fedha za ruzuku na fidia ya ada hutolewa kwa shule kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo au waliosajiliwa na shule husika, shule nyingi zinakabiliwa na ukata kutokana na kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi. Fedha inayopatikana inaruhusu kufanya mahitaji madogo madogo ya shule kama chaki, vitabu, na zana zingine za kujifunzia.

 Hali ni mbaya sana katika shule nyingi, baadhi ya shule zimefikia kushindwa kuchapa mitihani, wanafunzi wanaandikiwa mitihani ubaoni. Hii  hali ambayo ipo na haisemwi sana lakini ina athari kubwa. Serikali itizame upya kiwango cha fedha inachotoa mashule ili kiweze kukidhi mahitaji ya uboreshaji wa elimu.

Kuweka vigezo vipya vya kujiunga na chuo kikuu kumeminya pia mawanda ya elimu kukua. Nchi hii inawasomi wachache sana, sasa inapotokea vinawekwa vigezo vya kubana zaidi ili watu wasipate elimu ya chuo kikuu lazima ishangaze. Alama za kujiunga na chuo kikuu kwa wanafunzi waliotoka moja kwa moja kidato cha sita ni wastani wa D mbili au alama nne kutoka E mbili au alama tatu za awali.

Wizara ya elimu imetangaza vigezo hivyo mwaka huu na imedahili wanafunzi wa mwaka huu kwa kutumia utaratibu huo. Kanuni hizi mpya, ngumu na za ghafla zimeathiri ndoto za watu wengi kujiendeleza. Serikali imechukua maamuzi haya haraka ilipaswa itoe maamuzi haya mwakani au ingetangaza mwaka huu lakini yangeanza kutekelezwa mwakani ili watu wajiandae.

Ni hivyo pia watu wanaotaka kujiunga na chuo kikuu kwa cheti cha stashahada, sasa itabidi angalau wawe na ufaulu wa kuanzia daraja la 3. Bado maamuzi haya yanaathari hasi kwa watumishi waliopanga kujiendeleza mwaka huu. Mathalani walimu na wauguzi ni wahanga zaidi kwani wengi kutokana na mfumo wa elimu zao wengi huhitimu ngazi za stashahada wakiwa na chini ya daraja la tatu.

Wanafunzi wa kidato cha nne nao hawako salama, sasa daraja C linaanzia 45 kutoka 41 ya awali, daraja B linaanzia 65 kutoka 61 ya awali, Daraja A limeshushwa sasa litaanzia 75 mpaka 100. Ni jambo jema kwa uboreshaji wa elimu yetu lakini litaumiza watoto wetu hasa wanyonge. Watoto waliopandishiwa madaraja tukumbuke ni hawa ambao hawana walimu, hawana maabara, hawana maktaba, wanasoma kwa kukaa chini.

Kabla ya kupandisha madaraja serikali ilipaswa iboreshe kwanza mazingira ya utoaji elimu na ufundishaji ndipo mabadiliko haya yangekuwa na tija. Vinginevyo kuwapandishia madaraja wanafunzi ambao hawana walimu, maabara wala maktaba kadhalika hawana vitabu ni dhuluma. 

Wahanga zaidi wa mabadiliko haya ni watoto wa shule za kata, ambao walikuwa wanapata 41,42,43,44 na hivyo kujikuta wana daraja C leo wengi wanaoangukia hapo watajikuta wana D.
Kutoongeza mishahara kuna athari hasi. Licha Serikali ya awamu ya tano kurejesha ni dhamu ya kazi kwa watumishi hususani walimu kwa kiwango kikubwa, lakini kutowaongezea walimu mishahara kumenyong’onyeza sana mioyo ya walimu na kumevunja moyo wa uwajibikaji wa dhati.

Uwajibikaji uliopo hivi sasa kwa walimu ni wa woga tu. Walimu wengi wanawajibika kwa kuhofia kuchukuliwa hatua za kisheria lakini uwajibikaji kutoka ndani ya moyo wa mwalimu umepungua. Hali hii imetokana na mazoea ya walimu kuongezewa mishahara kila ifikapo mwezi wa saba kadhalika walimu walikuwa na matumaini makubwa sana na Rais wao kuwa awamu hii kulingana na ahadi zake angeboresha sana maslahi ya wafanyakazi. Kitendo cha kutoongezewa mishahara mpaka sasa kina athari, hivyo hii ni moja ya kasoro ya serikali ya awamu ya tano katika kuboresha walimu.

Mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu bado hali si shwari. Manung’uniko ni mengi kutoka kwa vijana wa vyuo, kinachoendelea kinakinzana kabisa na ahadi za Mh. Rais Magufuli wakati wa kampeni zake, ni kama ilikuwa ahadi ya kisiasa tu ili kujipatia kura kama ilivyoada ya wanasiasa wengi kutoa ahadi nyingi wasizoweza kutekeleza. Ubaguzi katika utoaji wa mikopo ni ukandamizaji wa wanyonge kwa kuwa sehemu kubwa ya wanufaika wa mikopo hii ni wanyonge.

Ukitoa mikopo kwa ubaguzi maana unawanyima wanyonge nafasi ya kujiendeleza, ukiwanyima nwanyonge nafasi ya kupata elimu basi unatengeneza tabaka katika jamii. Tabaka la wenye nacho na wasionacho.

Mr.Mwalimu Blog tunasema, ELIMU KWANZA. Elimu lazima kiwe kipaumbele cha kwanza katika nchi maskini kama Tanzania. Maendeleo yote ya kimiundombinu, kimawasiliano lazima yatangulie na maendeleo ya kielimu. Kuwa na nchi yenye barabara za lami mpaka uchochoroni lakini kuna watu wengi wasiojua kusoma na kuandika na kasoro.

Kadiri ya tafiti zaidi ya asilimia ishirini humaliza shule za msingi bila kujua kusoma na kuandika. Zaidi ya asilimia hamsini ya wanafunzi wakidato cha nne humaliza shule wakipata madaraja dhaifu yasiyowawezesha kuendelea. Pia walimu katika shule nyingi wanafundisha katika mlundikano mkubwa wa wanafunzi .Hizi ni changamoto za msingi ambazo serikali hii inapaswa itatue.

MWAKA MMOJA: JPM ALIVOIPANDISHA NA KUISHUSHA ELIMU.

Saturday, October 29, 2016

BASHE: MPIGANIA UBORESHAJI WA ELIMU NDANI NA NJE YA BUNGE

Mheshimiwa Bashe ni miongoni wa wanasiasa vijana machachari, wasioogopa na wenye upeo mpana wa kuelewa jambo.Pia ni miongoni mwa wanasiasa wachache wenye uwezo wa kujenga hoja kusimamia wanachokiamini.

 Mheshimiwa Bashe amekuwa mmoja ya wabunge wanaojipambanua waziwazi kuwa ni wapambanaji wa uboreshaji wa elimu. Bunge la kumi mpambanaji wa masuala ya kielimu alikuwa James Mbatia katika Bunge hili la kumi na moja namuona Bashe kutoka chama tawala. Mr.Mwalimu BLog, bila kuendekeza siasa nyepesi, Bashe anaipigania elimu kwa mawazo, kwa maneno, kwa matendo na hata kwa kile alichonacho.
 Baada ya kutambua kwamba elimu yetu bado haijawa bora kiasi cha kukidhi mahitaji yetu. Bashe kupitia ukurasa wake wa facebook ameanzisha kampeni ya kukusanya kura za wananchi ili kupeleka hoja Bungeni ya kutaka iundwe tume ya kitaaluma itakayo kusanya maoni juu ya mabadiliko ya elimu yetu. Jimboni kwake Nzega mjini, Bashe ameanzisha utaratibu utakao saidia kulipia gharama wanafunzi wote wa jimboni kwake watakaofaulu kujiunga na kidato cha tano. Katika kusisitiza jambo hilo Bashe alisema "Kutokana na idadi ndogo ya uhudhuriaji wa vijana elimu ya juu ya sekondari (kidato cha tano na sita) kwasababu ya wazazi kushindwa kulipa ada.
Nimeamua Kuwalipia ada wanafunzi wote wa jimbo langu la Nzega watakaofaulu kidato cha tano na sita kwenye shule za serikali, wazazi wajiandae na sare za shule na gharama nyinginezo. Ili kila mtoto apate nafasi ya kusoma na hata kufikia elimu ya juu." – Viongozi wengine waige mfano huu wa mheshimiwa Bashe katika kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu. Viongozi kuweni wabunifu katika kushughulikia changamoto za elimu.

Alishokifanya Bashe kitamfanya akumbukwe miaka mingi kuliko wabunge wanaogawa fedha kwenye sherehe za harusi za wapiga kura.

Wanafunzi kutumia namba moja ya mtihani katika kila ngazi ya elimu

Katika kuboresha na kurasmisha elimu Baraza la Mitihani limetangaza kutumia namba moja ya mtihani kwa ngazi zote za elimu. Ni babadiliko yenye tija. Chanzo ni Gazeti la Mwananchi

Kuanzishwa kwa mfumo wa namba maalumu ya usajili itakayotumiwa na wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi chuo ngazi ya diploma, kutasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi hewa.
Hayo yalitangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mitihani wa Necta, Khalifan Kabiki alisema utaratibu huo unafuta uliokuwa unatumika zamani ambapo mwanafunzi alipewa namba mpya kila alipofanya mtihani.
Mfumo mpya, utamtambua mwanafunzi kwa namba atakayosajiliwa nayo darasa la kwanza ambayo ataitumia katika maisha yake yote ya shule na taarifa zake zote zitakuwa humo.
Kabiki alisema mfumo huo ambao utakuwa wa kielektroniki, utasaidia uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa kutoa namba maalumu itakayomtambulisha mwanafunzi katika ngazi mbalimbali za mafunzo.
“Mfumo huu utasadia katika uandaaji na utoaji wa takwimu za wanafunzi katika ngazi ya shule, wilaya, mkoa na Taifa. Pia utarahisisha ufuatiliaji wa taarifa za matokeo ya kila mwanafunzi ili kuhakikisha wadau wa elimu wanapata ufahamu wa kutosha kuhusu ufundishaji na ujifunzaji,” alisema Kabiki.
Pia, mfumo huo utasaidia katika uhamisho wa mwanafunzi ndani na nje ya mkoa, kwani namba hiyo itakuwa ina taarifa zake zote muhimu na hakutakuwa na haja ya vielelezo vingine.
Kabiki alisema tayari mfumo huo umeanza kujaribiwa katika mikoa ya Mwanza na Ruvuma, na ifikapo Desemba utaimarishwa zaidi ili kuanzia Januari uanze kutumika nchi nzima.
Katika hatua nyingine, ofisa habari wa baraza hilo, John Nchimbi alisema Necta imeboresha mfumo wa usahihishaji mitihani ya Taifa kwa kuweka wasahihishaji kulingana na idadi ya maswali kwa kila somo.
Pia, Necta walisema wameimarisha udhibiti wa wizi wa mitihani na udanganyifu kwa kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.
“Usahihishaji wa sasa unatumia mfumo wa mnyororo kuepuka baadhi ya wasahihishaji kumkosesha mwanafunzi swali ambalo amelijibu kwa ufasaha kwa kuwa tu maswali yaliyotangulia alikuwa hajayajibu vizuri,” alisema.
Alisema mfumo wa kudhibiti wizi wa mitihani na udanganyifu umeimarishwa kutoka watahiniwa wadanganyifu 9,736 mwaka 2011 mpaka sifuri mwaka 2015 kwa elimu ya msingi.
Kwa kidato cha nne wanafunzi 3,303 walifanya wizi na udanganyifu huo kwa mwaka 2011 lakini idadi hiyo imepungua mpaka wanafunzi 87 mwaka 2015.

Nchimbi alisema mfumo huo umepunguza wizi na udanganyifu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kutoka 11 mwaka 2011 mpaka tano mwaka 2015.

Mungai; Kikwete alinitosa ili kuwafurahisha walimu

Joseph Mungai ni moja ya wanasiasa wakongwe wasioweza kusahaulika katika nchi hii, amewahi kuwa waziri katika wizara mbali mbali tangu serikali ya awamu ya pili mpaka ya nne. Ni mmoja kati ya mawaziri wa elimu wa Taifa hili ambaye alifanya kazi kubwa ya kuboresha elimu, pia anashutumia kwa kuharibu mfumo wa elimu nchini.Makala hii ilichapishwa na gazeti la Mwananchi, fuatilia mahojiano haya ufahamu kiundani.  
Kwa ufupi
Mungai, ambaye alikuwa ajibu tuhuma zilizoelekezwa kwake baada ya kustaafu siasa, amesema hata kiongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete hakutaka kumteua kuendelea kuongoza elimu kwa kuwa alitaka kufurahisha walimu waliokuwa wakimchukia kutokana na kuwabana.

 Joseph Mungai, ambaye alikuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni wa Serikali ya Awamu ya Tatu, amepinga vikali shutuma kuwa alishusha kiwango cha elimu, badala yake akairushia lawama awamu iliyofuata kuwa ilifanya maamuzi yaliyozorotesha sekta hiyo.
Mungai, ambaye alikuwa ajibu tuhuma zilizoelekezwa kwake baada ya kustaafu siasa, amesema hata kiongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete hakutaka kumteua kuendelea kuongoza elimu kwa kuwa alitaka kufurahisha walimu waliokuwa wakimchukia kutokana na kuwabana.
Mwanasiasa huyo mstaafu pia alipinga shutuma dhidi yake kuwa alifuta michezo shuleni, akisema hahusiki na suala hilo na alichokifanya ni kufuta michango ya mashindano ya Umiseta na Umitashumta na kutoa maelekezo michezo ifanyike nje ya muda wa masomo au mwishoni mwa wiki.
Mungai aliamua kuweka bayana masuala hayo wakati alipofanya mahojiano na mwandishi Luqman Maloto kuhusu mabadiliko makubwa ya elimu ambayo Serikali ya Awamu ya Tatu iliyafanya, lakini akaelekezewa lawama kuwa ndiye aliyeyafanya bila kushirikisha wadau na kusababisha kuanguka kwa elimu.
“Kama nilivyosema, nilijisikia vibaya kuona kazi nzuri tuliyoifanya chini ya uongozi wa Rais (Benjamin) Mkapa inabomolewa katika mwaka wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne,” alisema Mungai alipoulizwa alijisikiaje wakati anaona Baraza la Mawaziri linabadilisha uamuzi ambao waliufanya wakati akiwa Waziri wa Elimu.
“Nilisononeka sana. Pamoja na utu uzima wangu, sikusikilizwa. Niliwatahadharisha wahusika kuwa matokeo mabaya ya uamuzi huo watayaona baada ya miaka kadhaa. Matokeo yakawa kama nilivyosema. Baada ya mwaka 2007, matokeo ya mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne yalianza kushuka mwaka hadi mwaka.”
Mungai alisema katika kipindi hicho idadi ya wahitimu wanaofeli iliongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia kiwango cha juu mwaka 2012 wakati idadi ya waliofeli ilipofikia asilimia 60.
Alisema hata vyuo vikuu viliendelea na vinaendelea hadi sasa kupokea wanafunzi wasiojua vizuri Kiingereza kutokana na kufuta hata somo walilolianzisha la muundo wa Kiingereza kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu ya sekondari ili kuwaandaa na masomo ya chuo kikuu.
Mungai hakutaka kumlaumu mtu yeyote aliyeshika wizara hiyo, akisema katika kipindi cha miaka 55, takriban mawaziri 23 wameiongoza, ikiwa ni wastani wa miaka miwili kwa kila waziri na hivyo hakuna aliyepata muda wa kutosha.
Akizungumzia uamuzi ambao uongozi wake ulifanya wakati huo, Mungai alisema ni kubuni na kuanzisha Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) mwaka 2004 - 2009 uliopanua elimu ya sekondari kuwafikia angalau nusu ya rika lengwa la miaka 14-18.
“Tulianzisha vyuo vikuu vishiriki vya elimu vya Chang’ombe na Mkwawa kwa lengo la kufundisha walimu kwa ajili ya utekelezaji wa MMES. Upanuaji wa elimu ya sekondari ulipangwa kuendana na upanuaji wa mafunzo ya walimu wa sekondari,” alisema.
“Najivunia kufuta ada na kuifanya elimu ya msingi kuwa ya bila malipo na ya lazima kwa kila mtoto wa miaka saba hadi 13. Mzazi alibakia na wajibu wa kumpa mtoto wake malazi, mlo na mavazi. Nilipiga marufuku michango yote ya wanafunzi na wazazi wao. Michango ya ujenzi wa shule ni jukumu la wote wenye uwezo wa kufanya kazi; na siyo wazazi wa wanafunzi peke yao.”
Alisema wakati huo Serikali ilitoa ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi ya Sh10,000 kwa kila mwanafunzi, kutenga fedha kwa ajili ya michezo baada ya kufuta mchango wa Sh1,000 kwa ajili mashindano ya shule.
Mbali ya MMES, pia aliandaa na kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) 2002 - 2006 iliyotoa ruzuku za maendeleo na uendeshaji kwa wananchi wanaojenga na kuendesha shule. Kadhalika, alisimamia kupunguzwa kwa ada ya shule za sekondari za Serikali za kutwa kwa aslimia 50 kutoka Sh40,000 mpaka Sh20,000 na kuongeza ruzuku maradufu ya kuwasomesha sekondari bila ada, watoto wa familia zisizo na uwezo.
Alisema anajivunia pia kuanzisha mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), katika vyuo vyote vya ualimu, kusimamia marekebisho na kuanza kutekeleza mtalaa mpya wa sekondari uliounganisha masomo ya michepuo (ufundi, kilimo, biashara na sayansi kimu) na masomo ya kawaida uliotokana na mapendekezo ya Taarifa ya Mfumo wa Elimu ya Tanzania unaofaa kwa Karne ya 21 (The Tanzania Education System for the 21st Century).
Alipoulizwa kitu ambacho angetamani kuendelea kukisimamia wakati Serikali ya Awamu ya Nne ikiingia madarakani, Mungai alitaja maboresho ya elimu kwa kutekeleza mtalaa mpya.
“Lakini Rais Kikwete aliniteua kuwa Waziri wa Kilimo na baadaye kidogo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Niligundua baadaye kuwa lilikuwapo shinikizo la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) nisiteuliwe kuwa Waziri wa Elimu. Sikupendwa na walimu kwa sababu niliwabana mno,” alisema.

“Wakajibu mapigo kwa kumwambia mgombea urais wa CCM mwaka 2005 (Kikwete) kuwa wanamuunga mkono, lakini Mungai asiwe tena Waziri wa Elimu. Rais Kikwete akaamua kuwafurahisha zaidi walimu kwa kumteua aliyekuwaRrais wa Chama cha Walimu, Mheshimiwa Margareth Sitta kuwa Waziri wa Elimu baada yangu. Hivyo ndivyo siasa ilivyo.”

Thursday, October 27, 2016

Mwanafunzi ajifungua bwenini!

Mr.Mwalimu.Blogspot.com

Habari hii iliripotiwa na gazeti la mwananchi mwezi Septemba, tarehe kumi na tano. Ilihusu kisa cha kushangaza mwanafunzi kujifungua bwenini katika shule moja mkoani Dodoma.
Kama mzazi, mwalimu na mwanafunzi kuna cha kujifunza katika kisa hiki.Japo pia ni cha kuacha midomo wazi. Shule zenye wanafunzi wa kike lazima zijitahidi kuwapima afya za watoto mara kwa mara.

Dodoma. Mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Mbabala, Manispaa ya Dodoma, Helena Mpondo amejifungua mtoto ndani ya bweni.
Mwanafunzi huyo amejifungua mtoto mwenye afya njema kwa usaidizi wa walimu na baadaye aliitwa mganga wa zahanati ya jirani kwa ajili ya kumkata kitovu na msaada mwingine.
Helena, Ijumaa ya Septemba 2 saa tatu asubuhi alizidiwa na uchungu akiwa peke yake bwenini, lakini matroni na mwalimu mwingine wa kike waliwahi kufika eneo hilo na kumsaidia kujifungua salama.
Mkuu wa shule hiyo, Joram Mkwawa amesema siku ya tukio, saa tatu asubuhi aliitwa na walimu wenzake bwenini na alikuta binti huyo amejifungua.
“Nilichofanya niliwaambia waende zahanati na  nilituma pikipiki ya kumfuata mzazi wake ambaye alipofika, nilimkabidhi mwanawe kwa kuwa ni kosa kukaa na mtoto mwenye mimba,” amesema.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme alitoa taarifa kuwa manispaa hiyo ilikuwa na wanafunzi 51 wenye mimba na kati yao, 45 walikuwa wa shule za sekondari na sita wa shule za msingi.

BAADA YA BAKORA, KUPIGWA VIBAO NA KUDEKISHWA ,MWALIMU AJIANDAE KUPIGISHWA MAGOTI!

Mr.Mwalimu. Blogspot.Com

Si dhambi, si kosa la jinai wala si utovu wa nidhamu kwa mtumishi wa umma au mwalimu kugoma kutii maagizo ya muajiri au mkuu wake wa kazi pale maagizo hayo yanapokuwa yamekiuka sheria za kazi, haki za binadamu au yanapokuwa na dalili za udhalilishaji.

Ni wajibu na ni lazima kwa kwa mtumishi wa umma kutii maagizo ya muajiri au mkuu wake wa kazi, lakini hayo maagizo lazima yawe hayakinzani na sheria na taratimu za kazi na utumishi wa umma. Si haki wala vema kwa muajiri au mkuu wa kazi kutumia madaraka yake vibaya kwa kutoa maagizo au maalekezo ambayo yanakinzana na haki na taratimu za kazi.

Muajiri au mkuu wa kazi hayupo juu ya sheria za nchi, hana kibali cha kuvunja sheria za kazi, haruhusiwi kusigina sheria za utumishi wa umma wala hana ruhusa ya kukiuka haki za binadamu. Cheo ni dhamana, hakimpi mtu ruhusa wala mamlaka ya kumdhalilisha mtu wa chini yake, hakimpi mtu haki ya kudhalilisha utu wa binadamu.

Niliposoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna mwalimu ameamuriwa kudeki darasa na mkurugenzi wa halmashauri mbele ya wanafunzi, nilikataa kuamini, nilisema huu utakuwa ni uzushi tu au utani wa mitandaoni. Mpaka nilipojitahidi kuwasiliana na mtu mmoja wa halmashauri husika nikahakikishiwa kuwa ni ukweli.

Nikaketi chini kutafakari, nikakumbuka tukio la mkuu wa wilaya mmoja kanda ya ziwa hiyo hiyo kuwacharaza viboko walimu, nikakumbuka matukio kadhaa ya walimu kupigwa vibao na wakuu wake wa kazi likiwemo la mwishoni mwa mwaka jana mkoani Dodoma.

Nikakumbuka shuhuda za baadhi ya walimu jinsi wanavyoshambuliwa kwa lugha chafu na maneno ya kuudhi na wakuu wao wa kazi katika halmashauri, nikatafakari madai ya walimu yanavyopuuzwa, kisha nikatafakari wanaofanya hivyo nao walifundishwa na walimu hawa hawa wanaowadhalilisha leo. Nikahitimisha kwa huzuni nyingi kuwa ni kweli tenda wema nenda zako.

Nikiri kauli ya Rais wa chama cha walimu ,Gration Mkoba, wakati akihojiwa na gazeti la Raia mwema katika siku ya mwalimu duniani, alisema ualimu ni “kazi ya kitume”.Ni kazi ya kutenda wema na kwenda zako usingoje shukrani, fundisha kwa moyo lakini usitegemee malipo sawia wala heshima sawia. Wengine utawafundisha watakudekisha kesho na wengine watakukumbuka kwa wema na baadhi utafundisha watalitumikia taifa vizuri hata utajivunia.

Kwa kweli baada ya kutafakari sana nikajikuta inanijia picha ya walimu wakiwa wamepigishwa magoti na mkuu wao wa kazi! Usishangae, ndiyo kitu ambacho nakiona kikimtokea mwalimu huko tuendako. Kama mwalimu anachapwa viboko, anapigishwa magoti na anapewa adhabu ya kusafisha darasa basi mwalimu ajiandae kupigishwa magoti ofisini kwa afisa elimu, mkurugenzi au kwa mkuu wa wilaya!Wasomaji wa Mr.Mwalimu.blogspot.com ,hadhi ya walimu iko mashakani!

Vitendo tunavyovishuhudia sasa kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano na habari ni vichache kati ya vingi ambavyo walimu wanatendewa hasa maeneo ya ndani ndani. Mengi hayaripotiwi lakini yanatokea, ukihoji walimu utasimuliwa mengi ambayo hutaamini.

Ni kwa bahati mbaya sana vitendo vya kidhalilishaji kama kuchapwa viboko, kupigwa makofi, kutamkiwa maneno machafu na kudekishwa,wanatendewa walimu tu, walimu ambao ndiyo asilimia zaidi ya sabini ya watumishi wa umma ndiyo wahanga wakuu wa vitendo vya udhalilishaji. Na ni walimu ndiyo waliofundisha hao wanaodhalilisha walimu sasa.

Kwa kuwa vitendo vya kudhalilisha walimu vinaongezeka, vinazoeleka, vinaanza kuwa ni vya kawaida kiasi kwamba mwalimu anaanza kupewa hadhi ya mwanafunzi kwamba ni mtu wa kuadhibiwa pale anapokosa. Na kwa kuwa Chama cha walimu hakina hatua za zaidi za kuchukua dhidi ya vitendo hivi zaidi ya kumtaka mdhalilishaji aombe msamaha na kutoa tamko la kimaneno la kupinga vitendo hivi.

Kadhalika kwa kuwa vitendo hivi havijawahi kukemewa hadharani na waziri yoyote anayehusika na elimu au hata katibu mkuu wa wizara inayohusika na elimu, naomba mwalimu achukue hatua. Pamoja na hilo niviombe vyama vya  walimu kote nchini, viache ukasuku, visiishie tu kudai madai ya walimu, visihishie tu kudai nyongeza, visiishie tu kukata asilimia mbili ya mishahara ya walimu. Vitoe elimu ya kujitambua kwa walimu. Vifundishe walimu haki zao kama watumishi wa umma na kama wafanyakazi. Hivi kuna faida gani kuwa mwalimu ambaye unalipwa vizuri lakini huna hadhi, unadhalilishwa kila siku?

Heshima ya mtu inalindwa na mtu mwenyewe, hadhi ya mwalimu italindwa kutetewa na mwalimu mwenyewe. Mwalimu usingoje CWT wakutetee haki yako unao uwezo wa kujitetea mwenyewe. Simama imara na jiamini. Nasema mbele za Mungu ingekuwa ni mimi mkurugenzi amenipa amri ya kudeki ningesimama kumtaza usoni tu bila kumjibu kitu.

Hata angerudia amri hiyo mara kumi nisingetii, bali ningebaki kumtiza bila wasiwasi wala kuogoba, ningemtazama usoni kwa heshima zote kwa kuwa ni mkuu wangu wa kazi , nisingemuonyesha sura ya dharau, wala nisingekimbia lakini nisingetafuata ndoo ya maji wala tambala la kudekia liliko. Kutii kila maagizo unaweza jikuta una tii maagizo ya mtu aliyelewa, alafu wewe ukabaki kudhalilika na akili zako timamu.

Binafsi najiuliza maswali mengi sana, Nchi hii imepita mikononi mwa marais wa tano mpaka sasa, sijawahi sikia marais hao katika zama zao waliwahi kumdhalilisha mkuu wa mkoa, mkurugenzi wa shirika la umma , mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa halmashuri wala mkuu yoyote wa idara fulani. Sasa hawa wanaodhalilisha walimu wanatoa wapi ujasiri huo wa kufanya mambo ambayo hata Rais mwenyewe hafanyi?

Kuna wakati na mazingira ambayo mtu ukitendewa udhalilishaji, wewe uliyedhalilishwa ndiye unakuwa unastaahili kulaumiwa. Kukubali kuonewa si utii, ni nidhamu ya woga ambayo haina faida. Fikiri kama yule mwalimu angegoma kudeki lile darasa na akaripoti ngazi za juu ingetokea nini.

Nasema wazi mwalimu aliyekubali kudekishwa mbele ya wanafunzi alikosea sana na ni dalili kuwa wafanya kazi wengi wa umma hasa walimu hatujui haki zetu. Ndiyo maana hatusikii wauguzi, madaktari, maaskari, maafisa maendeleo, mabwanamifugo wala wahasibu wakifanyiwa hivyo vitendo hivyo bali walimu tu ndo wanaofanyiwa hivyo.

 Mwalimu una haki ya kukataa kutii maagizo ya mkuu wako wa kazi au muajiri wako kama unaona amekusudia kukudhalilisha.  Mwalimu fahamu una sheria zinazokulindwa, usikubali kupelekwa pelekwa kama roboti.

Kuonewa au kudhalilishwa mara moja si mbaya ile kuendelea kudhalilishwa ni uzembe. Mtetezi wa kwanza wa taaluma ya ualimu, utu wa mwalimu, na haki za mwalimu ni mwalimu mwenyewe. Kinyume chake naweza sema adui wa kwanza wa utu na hadhi ya  mwalimu ni mwalimu mwenyewe, taaluma ya ualimu itetewe na walimu wenyewe.

Mwalimu lazima utambue kuwa hakuna mtu kutoka nje ambaye atakutetea kwa kiwango kikubwa kama ambavyo unaweza kujitetea wewe mwenyewe. Bila kujitetea wenyewe hadhi ya walimu na ualimu itashuka kila leo na visa vya udhalilishaji vitaongezeka kama tunavyosikia kiasi cha kuanza kuzoeleka kuwa walimu ni kawaida kutendewa vibaya.

MZIZI WA ELIMU NI MWALIMU. MWALIMU KATAA KUDHALILISHWA.MR.MWALIMU.BLOGSPOT.COM ELIMU KWANZA.

Monday, October 24, 2016

MRISHO GAMBO: KWA NINI WALIMU WANAICHUKIA SERIKALI

Nov 23, 2013 ,gazeti la kila wiki Raia Mwema lilichapisha makala hii, makala iliandikwa na Mrisho Gambo, miongoni mwa wanasiasa na viongozi vijana wenye harakati nyingi chanya. Wakati anaandika alikuwa mkuu wa wilaya ya Korogwe, huku alipigania sana maslahi ya walimu, baadaye alihamishiwa Uvinza, Arusha na sasa ni mkuu wa mkoa wa Arusha. Ni mtu mwenye msimamo, mwenye kukuiamini anachosema na kukiishi. Naomba niirejsehe makala yake kwa kuwa vingi alivyosema vinasadifu changamoto za sasa za walimu kadhalika yeye ameendelea kuwa mtetezi wa walimu.

LEO nimeona nami nianze kuweka mawazo yangu kwenye maandishi. Japokuwa kwa sasa ni kiongozi wa serikali, naamini nafasi hiyo haininyimi fursa ya kutoa mchango wangu wa mawazo kwa mustakabali wa taifa langu.

Nimekuwa nakiandika kwenye mitandao ya kijamii kama facebook pamoja na kutoa hotuba mbalimbali kwa watumishi na wananchi wilayani Korogwe. Nimeona niandike baadhi tu ya changamoto zinazowakabili walimu kwa kuwa nimekuwa nikijiuliza sana; mbona serikali inafanya mambo mengi kwa walimu lakini bado kuna baadhi ya walimu wanaichukia serikali yao?

Ninaandika masuala ambayo naamini yangefanyiwa kazi walimu wasingekuwa na manung’uniko makubwa. Sitazungumzia lile la kutaka kupandishwa mshahara kwa asilimia 100 ambalo kwa sasa naamini halitekelezeki.

Baada ya kutafakari yote hayo nimeona niandike uchambuzi ambao kwa kiasi kikubwa utazungumzia changamoto za kiutumishi za walimu wetu.

Kuwapandisha walimu madaraja

Hii ni changamoto inayowakabili walimu wetu Tanzania nzima. Wakati mwingine inasababishwa na ufinyu wa bajeti ya serikali pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji serikalini. Serikali mara nyingi imekuwa ikitoa maelekezo ngazi za halmashauri lakini mara nyingi yamekuwa hayafanyiwi kazi kwa uzito unaostahili.
Katika kipengele hiki nitatoa mfano hai,  nina ushahidi wa uzembe uliofanywa na Halimashauri ya Mji Korogwe kwenye bajeti ya mwaka 2012/2013. Walisahau kuwapandisha madaraja walimu zaidi ya 30 wa sekondari walioajiriwa mwaka 2009.

Walimu hao walitakiwa kupanda daraja kwenye bajeti ya mwaka 2012/2013, lakini wakasahaulika kwa uzembe pamoja na serikali kutoa muongozo kuwa watumishi wote wanaostahili kupanda daraja wapande wote.

Lakini wao wakawaweka kwenye bajeti ya 2013/2014 badala ya 2012/2013, nini tafsiri yake? Walimu hawa wataachwa nyuma kwa mwaka mmoja kimaslahi na walimu wenzao walioanza kazi pamoja, ikiwa ni pamoja na kutolipwa malimbikizo yao kwa sababu serikali ilikwishatoa muongozo kuwa wote wawekwe kwenye bajeti.

Kitendo kama hiki cha uzembe wa watu wachache (mkurugenzi na wenzake) kinawafanya walimu kuichukia serikali yao. Pia kuna malalamiko ya walimu kushushwa madaraja bila hatia yoyote pamoja na wengine waliokuja baada ya wao kuajiriwa, kupanda daraja na wa zamani kubaki pale pale.

Hii ni changamoto kubwa na jambo hili ni kilio cha walimu wilayani Korogwe hadi leo. Halimashauri ya Korogwe Vijijini hawana tatizo hili japokuwa wao wana eneo kubwa la utawala (Kilomita za mraba 3574 wakati za halmashauri ya mji ni kilomita za mraba 212), wao walifanikiwa kuwapandisha daraja walimu wote walioajiriwa mwaka 2009. Hili linawafanya walimu waichukie serikali yao.

Malimbikizo ya madeni ya mshahara kwa walimu

Suala hili linahitaji kubadili mazoea katika utendaji. Kwa mtazamo wangu serikali kuu na serikali za mtaa zote ni serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lazima halmashauri zetu zibadilike na kubeba jukumu hili la malimbikizo ya madeni ya walimu ya mishahara na si kukusanya tu na kupeleka serikali kuu.
Sasa umefika wakati watenge pesa kutokana na mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kumaliza madeni ya walimu.

Nimekuwa nikitoa mfano kuwa kama wameajiriwa walimu 30 wa sekondari kwa ngazi ya shahada  ambao mshahara wao ni 532,000 kwa mwezi kwa kila mmoja kwa walimu wa shahada, jumla yake hapa ni shilingi 15,960,000.

Unakuta halmashauri  wanalipeleka deni hilo serikali kuu na inachukua zaidi ya miaka mitatu bila kulipwa, kumbe halmashauri wangeweza kulipa kupitia mapato ya ndani na kama serikali kuu italeta, halmashauri itawataka walimu walipe pole pole kwa kuwakata kwenye mishahara yao.

Hii ni muhimu kwa kuwa utakuta mwalimu katoka Kigoma na kupangiwa kazi Korogwe ambako hana ndugu na hakuna nyumba ya serikali ya kufikia. Mwalimu huyu na wenzie utakuwa umewaharibu kisaikolojia na wataiona serikali yote haina maana kwa sababu ya shilingi 15,960,000. Jambo hili lina wafanya walimu waichukie serikali yao.
Kukosekana motisha kwa walimu wa sayansi

Kwanza naunga mkono agizo la Rais Jakaya Kikwete, pamoja na jitihada za serikali na wananchi kujenga maabara kwa kila sekondari ya kata nchini. Wilayani Korogwe tunaendelea kwa kasi na mchakato huu.
Jitihada hizi zitatuondolea changamoto ya upungufu wa walimu wa sayansi mbele ya safari. Kwa sasa tunatakiwa kuwapa motisha walimu wa sayansi kutokana na uchache wao unaosababisha kupangiwa vipindi vingi kuliko wenzao wa masomo ya sanaa.

Mfano, kwa wiki mwalimu wa sanaa anakuwa na vipindi vinne hadi saba, wakati mwalimu wa sayansi anakuwa na vipindi kati ya 22 hadi 30 bila motisha yoyote. Mwalimu huyu lazima akate tamaa na ajione kama ananyonywa na serikali yake.

Jambo hili pia linawafanya walimu wa sayansi waichukie serikali yao. Lazima tutafakari namna ya kuwapa motisha walimu wetu wa masomo ya sayansi. Ni dhahiri, jambo hili linawafanya walimu wa sayansi waichukie serikali yao.

Aina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza

Tunapeleka wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi waliopata alama 70 chini ya 250 ambayo ni sawa na asilimia 28 ambayo ni alama D.

Mwaka huu kwenye Mock wamesema angalau alama 100 chini ya 250 ambayo ni sawa na asilimia 40 na yenyewe kwangu pia ni D, kwa sababu nimezoea kuwa C inaanzia asilimia 41. Humu humu inasemekana wamo wasiojua kusoma na kuandika, maana hata hesabu zenyewe ni za kuchagua, inakutosha kuambia eti umefaulu.

Kwa mwanafunzi huyu pia mwalimu anawekewa Big Result Now (BRN). Kama anaingia kidato cha kwanza amefeli maana kapata D, tunatarajia nini kidato cha nne? Sisi tuliosoma teknolojia ya kompyuta tunasema kinachoingia ndicho kinachotoka.

Tunahitaji kupitia upya utaratibu wetu wa kuwapata wanafunzi wetu wa kidato cha kwanza. Lazima wizara iweke mikakati madhubuti kwenye jambo hili, ili kumsaidia Rais wetu aache alama ya kukumbukwa na Watanzania kwenye dhana ya BRN.
Mafunzo kwa walimu

Mafunzo kwa walimu ni muhimu sana. Kwenye vyuo vya ualimu walimu hufundishwa mbinu za kufundishia, ambazo kwa mazingira ya sasa zinahitaji kuboreshwa zaidi.
Ni vema serikali ikaliangalia vema jambo hili ili walimu wetu waendane na mahitaji ya elimu yetu ya sasa.

Nyumba za walimu

Nyumba za walimu ni muhimu sana. Kuna maeneo mengine hata nyumba za kupangisha walimu hakuna kutokana na mazingira yenyewe. Lazima halmashauri itambue maeneo kama haya wakati wa kutekeleza jambo hili.

Kwenye bajeti ya mwaka huu kila halimashauri itapewa shilingi milion 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu. Fedha hizi lazima zisimamiwe vizuri na tuachane na mambo ya wakandarasi ili tupate nyumba nyingi zaidi jambo ambalo limechangia halmashauri zetu kuwa mchwa na shamba la bibi.

Walimu kusimamia mitihani

Kulikuwa na utaratibu uliozoeleka kwa kikundi fulani cha walimu tu ndio waliokuwa wakisimamia mitihani. Kipindi fulani niliwahi kuuliza hivi kuna walimu waliosomea somo la kusimamia mitihani kiasi ambacho wengine wanakosa sifa hiyo?

Kama vigezo ni kuwa kazini miaka mitatu na kuwa na TSD namba pamoja ma vigezo vingine, sasa kwa nini kila mwaka wajirudie hao hao? Jambo hili linafanya walimu waichukie serikali yao.
Walimu kulipia vitambulisho vya kazi

Kumekuwa na utaratibu wa kuwalipisha walimu shilingi 2,000 kwa ajili ya vitambulisho, kitambulisho ni mali ya mwajiri ambaye ni serikali. Kuwalipisha walimu ni kinyume cha utaratibu. Halimashauri zimekuwa zikiwachangisha walimu wetu.

Nauliza, mbona vitambulisho vya taifa ni gharama zaidi lakini serikali inatoa bure? Jambo hili linawafanya walimu waichukie serikali yao.
Walimu kulipia ujazaji wa fomu za OPRAS

Kumekuwa na utaratibu wa baadhi ya halmashauri nchini kuwataka walimu walipie gharama za photocopy za fomu za Opras. Fomu hizi ni mali ya serikali kwa ajili ya kupima utendaji kazi wa watumishi. Kumlipisha mwalimu kwa ajili ya fomu hizi ni kinyume cha utaratibu. Jambo hili linawafanya walimu waichukie serikali yao.

Uhaba wa vitendea kazi

Hapa serikali inastahili pongezi maana imefanya kazi kubwa kwa upande wa vitabu. Jitihada zinatakiwa ziongezeke kwenye upande wa ofisi za walimu na maeneo mengine.
Nimegundua mambo kama haya ambayo yapo ndani ya uwezo wa serikali yanachangia kuongeza chuki kwa walimu dhidi ya serikali yao. Umefika wakati sasa wa kuwachukulia hatua za makusudi watumishi wote wanaoikwamisha serikali na watumishi wenzao, kwa sababu kila mwaka changamoto zimekuwa ni zilezile.

Sasa kwenye elimu tunazungumzia (Big Results Now- BRN – (Matokeo makubwa sasa), lakini kwa kweli bila kuangalia maslahi ya walimu itakuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
BRN kwenye elimu ni zaidi ya mjadala wa daraja sifuri (division 0) na daraja la tano (division 5) kwenye jamii yetu. BRN naikubali kwa asilimia 100, baadhi ya watendaji wa serikali tusikubali kuipotosha dhana hii nzuri kwa wananchi na kudhoofisha juhudi za serikali yetu, badala yake tujielekeze kwenye matatizo ya msingi ya walimu wetu.

Mwandishi wa makala hii, Mrisho Gambo ni Mkuu wa Wilaya Korogwe(sasa mkuu wa Mkoa wa Aruusha), mkoani Tanga na msomaji wa gazeti hili. Anapatikana kwa simu: +255766757575. barupepe; mrishogambo@gmail.c  )

Friday, October 21, 2016

Kanda ya Ziwa bila maji: Ukosefu wa maji unavyoathiri elimu

 Mr.Mwalimu Blog

Kero ya maji katika kanda ya Ziwa ni jambo la kustaajabisha sana kwa watu ambao hawajawahikufika ukanda wa ziwa, kwa sababu wao picha walioyonayo kichani ni tofauti na hali halisi. Wengi tunaposema kanda ya ziwa kuna shida ya maji hawaamini lakini ndiyo ukweli.

Mikoa ya Mwanza, Geita, Mara na Simiyu ni moja ya mikoa yenye uhaba mkubwa wa maji licha ya kulizunguka ziwa Victori ambalo lingeweza kuwa chanzo mbadala cha maji. Wakazi wengi wa maeneo haya wanatumia maji yasiyo salama na machafu. Mathalani, Mkoa wa Mara ambao umepitiwa na Ziwa victori una kero kubwa ya maji hata kwa wakazi wanaoishi jirani na ziwa hilo.

Mkoa wa Mara na wilaya zake kama Rorya, Tarime, Bunda, na Serengeti bado hawajanufaika na uwepo wa Ziwa Victoria kama chanzo cha maji. Mkoa huu ambao pia una chanzo kingine kikubwa cha maji kama kingewekewa mikakati mizuri ambacho ni Mto Mara, wakazi wake hawana uhakika wa kupata huduma ya maji!

Inashangaza kama Mufindi ilivyoshangaza kuwa miongoni mwa wilaya ambazo wanafunzi wanakaa chini kutokana na ukosefu wa madawati licha ya kwamba Mufindi ndiyo wilaya inayoongoza kwa kuzalisha miti, mbao na kusambaza kwa nchi nzima! Na kanda ya ziwa ni hivyo maji ya Ziwa victori yamepelekwa mkoa wa Shinyanga, ambako ni mbali sana na ziwa lilipo lakini Geita, Mara, Simiyu ambako ndiko ziwa liliko hakuna maji.

Kama ilivyo mikoa mingine ambayo haina mito wala maziwa, wakazi wa kanda ya ziwa wanasumbuliwa na kero ya maji kama wao. Mathalani Maeneo ya jirani na Shirati, na kata kadhaa za wilaya ya Rorya, Komaswa kwa upande wa Tarime, maji yanauzwa mapaka shilingi mia 400 na 500 kwa lita ishirini. Na maji yanayonunuliwa kwa bei hiyo bado si salama.

Mikoa ya kanda ya ziwa ambayo wakazi wake wengi ni wafugaji, wanategemea maji ya mvua, maji yaliyovunwa kupitia mvua yakiisha, wakazi wa kanda ya ziwa wanatumia maji ya kwenye malambo ambayo pia yanatumika kunyweshea mifugo.

Ukosefu huu wa maji  unaathiri mfumo mzima wa maisha ya wakazi wa kanda ya ziwa kwa sababu bila maji hakuna uhai, hakuna afya bora, hakuna furaha ya maisha. Fikiri baadhi ya maeneo ya mikoa ya kanda ya Ziwa wakazi wake wanatumia zaidi ya saa nne ili kupata maji toka umbali wa kilometa  zaidi ya kumi.
Uhaba wa maji unaathari kubwa sana katika sekta ya elimu, wanafunzi wa mikoa ya kanda ya ziwa wanaumizwa zaidi na hali hii, kwa kweli ni wahanga wa kuu wa kero ya ukosefu wa maji.

Penye ukosefu wa maji safi na salama, hapana afya bora. Magonjwa ya tumbo ni moja ya changamoto kubwa sana kwa afya ya wanafunzi wa kanda ya ziwa. Wanafunzi wengi huugua magonjwa ya tumbo hivyo kushindwa kuhudhuria masomo. Katika siku 192 za masomo kwa mwaka, zaidi ya siku thelathini zinapotea bila kuhudhuria masomo kutokana na kusumbuliwa na magonjwa ya tumbo!

Kero ya maji inasabisha mahangaiko makubwa kwa wanafunzi, hii ni kwa sababu shule nyingi hazina visima wala mabomba ya maji. Katika shule hizi wanafunzi hulazimika kubeba vidumu vya maji kutoka nyumbani ili kumwagilia maua na miti ya mazingira ya shule pia kwa ajili ya huduma ya choo. Wakati mwingine wanafunzi wanatumia muda mrefu kwenda kufuata maji mara baada ya kuripoti shule kiasi wanakosa vipindi vyote vya asubuhi.

Ukosefu wa maji unaathiri pia ratiba ya wanafunzi kujisomea nyumbani mara baada ya kurejea kutoka shule. Ili mwanafunzi afanye vizuri katika masomo lazima apate muda wakutosha kujisomea baada ya saa za shule.

Wanafunzi wengi wa kanda ya ziwa hawana muda wa kujisomea, maana mara tu wanaporejea kutoka shule wanafanya safari nyingine ndefu na yenye mikiki mikiki mingi kwenda kufuata maji. Huko licha ya kusafiri umbali mrefu hukutana pia na foleni kubwa kiasi hupoteza saa nyingi zaidi ambazo wangeweza kuzitumia katika masomo.

Kero hii ya maji inaathiri pia walimu, walimu waliopelekwa na serikali maeneo haya ya kanda ya ziwa, wanakatishwa tamaa pia na hali ya ukosefu wa maji. Gharama kubwa ya kupata maji, muda mwingi unaotumika ili kupata maji vinaathiri ufundishaji wa walimu katika shule zao.

 Wanafunzi wanakosa masomo kwa sababu walimu wanatumia muda mwingi kufuata maji. Hali hii pamoja na maji yenyewe kuwa si masafi na salama imechangia walimu wengi kutopendelea kufanya kazi katika vijiji ambavyo vinashida ya maji. Baadhi wamelazimika kuhama haraka au hata kuacha kazi.

Usafi binafsi wa wanafunzi kama vile kuoga, kufua na kadhalika vinakuwa vigumu kwa wanafunzi kwa sababu ya ukosefu wa maji. Mwanafunzi anatakiwa pia kujifunza kujiweka nadhifu, ufundishaji unadhifu kwa vitendo kwa vijana wetu unakuwa mgumu kwa sababu ya shida ya maji. Kuna wakati mwanafunzi anavaa ngua chafu inabidi tu mwalimu uvunge maana unajua kinachomsibu.

Ushauri wangu kwa viongozi wa mikoa ya kanda ya Ziwa na wilaya zake, wakuu wa halmashauri na madiwani, wabunge wote bila kujali wajimbo ama wa kuteuliwa suala la ukosefu wa maji liwe ajenda kuu katika vikao na litekelezwe kwa vitendo.Ni aibu na uzembe kanda ya ziwa kukosa maji.\

Pia wananchi wa kanda ya ziwa ni wakati wakudai maji bila kusita bila uitikadi wa vyama, katika kila kikao tunachokaa na viongozi wetu tuwaambie MAJI KWANZA.MR.MWALIMU.BLOGSPOT.COM, ELIMU KWANZA.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...