Uhitaji mkubwa wa walimu kuhama kwa njia ya uhamisho maalumu
au kubadilishana halmshauri umetoa mwanya kwa watu kujipatia fedha hisivyo
halali kutoka kwa walimu wenye uhitaji huo.
Watu hao wenye nia ya kujipatia fedha kwa njia isiyo
halali, tayari wamewawaingiza mjini baadhi ya walimu, kwa kuwatoza kiasi cha
fedha kinachoanzia laki moja mpaka laki nne. Si hadithi, tayari kuna walimu
wamelizwa hela bila kukidhiwa haja yao.
Mmoja ya mwalimu ambaye ametapeliwa na walimu hao kiasi cha
shilingi laki moja kati ya laki tano walizokubaliana ili kukamilisha uhamisho
huo, anasema alikutana na madhira hiyo baada ya yeye kutangaza uhitaji wake wa
kutafuta mtu wa kubadilishana nae kupitia kundi la mtandao wa facebook ambalo
walimu hutumia kutangaza uhitaji wao wa kuhama kisha utaja maeneo
wanayopendelea kuhamia na kuweka mawasiliano yake.
Baada ya kuandikika ujumbe wenye nia ya kutafuta mtu wa
kubadilishana nae na kuweka maeneo anayoyapendelea pamoja na kuweka mawasiliano
yake, siku ya pili alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi
wa TAMISEMI. Mtu huyo alijitahidi kuongea kwa lugha tamu katika hali ya
kuonesha kuwa yeye ni kigogo katika wizara hiyo.
Katika maelezo yake alimtaarifu huyo mwalimu kwamba yuko
wizarani na wanaratibu uhamisho maalumu kwa walimu ili kuweka uwiano mzuri wa
wanafunzi katika mikoa. Hivyo kuna walimu wanahitajika wahamishwe kutoka mikoa
mbali mbali wapelekwe halmashauri za Mtwara, Morogoro Manispaa, Kinondoni na
Ilala.
Baada ya kupewa maelezo hayo mwalimu huyo aliambiwa kama ana
uhitaji, atume fedha taslimu laki tano ili kigogo huyo awahonge wajumbe wenzake
wapitishe jina la mwalimu huyu liwe miongoni mwa majina yatakayohamia Manispaa
ya Morogoro ambako mwalimu huyo alionesha nia ya kutaka kwenda.
Mwalimu mwenye uhitaji wa kuhama aliomba apunguziwe, lakini
kigogo huyo wa uongo hakukubali, mwishowe wakaafikiana kuwa mwalimu huyo atoe
shilingi laki moja na kiasi kilichobaki atamalizia mara atakapopata barua ya
uhamisho.
Mwalimu alituma hela hizo laki moja, lakini mara baada ya
kuzituma muhusika akazima simu, hakupatikana, alikuja kupatikana siku ya pili.
Cha ajabu baada ya kupatikana akaibuka na dai lingine la kuongezewa hela,
mwalimu alivyokuwa mgumu kuongeza kiasi cha fedha, kigogo huyo akadai fedha
hiyo haitoshi kumuhamisha hivyo asubiri mwakani!
Muda si mrefu laini ile ya simu haikupatikana tena, jitihada
za kuziokoa zile fedha kupitia kuwasiliana na huduma kwa wateja ziligonga
mwamba baada ya kuambiwa mtu huyo amekwisha toa kiasi hicho cha fedha.
Walimu mlio katika uhitaji wa kuhama make chonjo maana kuna
wimbi kubwa la utapeli wa namna hii,wapo hata watu wanaotuma ujumbe wa maneno
kusema kuna mtu anaweza kukusaidia kuhama. Hao wote ni wale wale, tukumbuke pia
uhamisho umesitishwa mpaka hapo serikali itakapotanngaza tena.
0 Comment to "UTAPELI: UHITAJI WA UHAMISHO KWA WALIMU WAGEUKA KITEGA UCHUMI!"
Post a Comment
Post a Comment
1410