Viongozi lazima kutambua mahitaji ya jamii kwa wakati husika. Mbunge huyu
kafanya kitu sahihi kwa wakati sahihi. Wanafunzi zaidi ya mazingira mazuri ya
kujifunzia ,wanahitaji ukaribu, wanahitaji kutiwa moyo na kuwaambia tuko
pamoja.Hongera Mbunge wa Kibiti.Wabunge wengine waige. Chanzo cha habari hii ni
Gazeti la MWANANCHI.
Kibiti. Mbunge wa Kibiti, Ally Seif Ungando ametoa vifaa mbalimbali vya kufanyia mtihani wa kidato cha nne na chakula kwa wanafunzi 800 kutoka shule kumi na moja wanaotarajia kuanza mtihani wa Taifa kesho.
Akizungumza katika utoaji wa vifaa hivyo katika Shule ya Sekondari ya
Zimbwini, Ungando amesema lengo la kutoa vitu hivyo ni kuwaondolea wanafunzi
usumbufu wa ukosefu wa vifaa hivyo na chakula wakati mitihani yao.
Ungando amesema ametoa vitu hivyo baada ya kubaini kuwepo kwa mapungufu ya
vifaa vya kufanyia mtihani kwa baadhi ya wanafunzi na wengine kutokuwa na
uhakika wa kupata chakula wakati wa kipindi cha mtihani yao.
"Vifaa hivi vya kufanyia mtihani na chakula hiki, nimevitoa ili
kuwaondolea usumbufu wa uhitaji katika kipindi cha mitihani yenu mnayotarajia
kuianza Jumanne," amesema.
Mbunge huyo ametoa mchele, maharage, mafuta ya kula, rula, kalamu za wino
na mkaa pamoja na nyembe vilivyogharimu zaidi ya shilingi milioni tano.
Shule zilizopokea vifaa hivyo ni Zimbwini, Mchukwi, Mlanzi, Ruaruke,
Kikale, Mtanga Delta, Wama, Nyamisati, Mlanzi, Mjawa na Msafiri.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Zimbwini, Harieth Mhadu amesema vifaa hivyo
vitaongeza molari zaidi wa wanafunzi hao kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
0 Comment to "Mbunge wa Kibiti awapa morali kidato cha nne"
Post a Comment
Post a Comment
1410